Ndani ya Exness

Kujitolea kwa Exness kufanya ulimwengu kuwa mahali bora

Na Paul Reid

5539_Exness_Blog Banner_600x400_EN (3).png

Tunajua kuwa masharti ya biashara ya Exness yanaweka viwango vipya katika sekta ya biashara na hii ndiyo sababu kuu ya traders kusalia, lakini kuna mengi zaidi kuhusu Exness. Timu yetu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ilikuwa na matokeo chanya kwa ulimwengu katika 2024, ambayo yalipelekea kupata tuzo tano katika Tuzo za Biashara zenye Uwajibikaji za Kupro (RBA) za 2024.

Mipango yetu yenye athari chanya ilitambuliwa katika kategoria nyingi:

Mazingira - Mipango ya Kuzima moto (Tuzo la Dhahabu)

Mpango wetu mpana wa kuzuia na kukabiliana na moto wa msituni ulipata heshima kubwa. Mpango huu ulijumuisha kutoa magari ya kuzima moto, kushirikiana na Idara ya Misitu na mashirika ya kieneo kwa ajili ya upandaji miti upya na kufanya kazi na Taasisi ya Teknolojia ya Kupro ili kutengeneza ndege zisizo na rubani zilizoundwa kulingana na eneo la Kupro kwa ajili ya kutambua moto mapema.

Ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (Tuzo ya Dhahabu)

Tulipongezwa kwa ushirikiano wetu na mashirika ya serikali na mashirika ya kieneo kushughulikia changamoto kubwa za mazingira. Kwa kuongeza uwezo wa kuzima moto na ubunifu kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya ndege zisizo na rubani, tumesaidia kuimarisha juhudi za kuzuia moto wa msituni.

Uwekezaji wa muda mrefu (Tuzo la Fedha)

Kujitolea kwetu kwa uendelevu wa mazingira na maendeleo ya jamii pia kulitambuliwa. Pamoja na mipango ya kuzima moto, tumejenga uhusiano wa muda mrefu na Idara ya Misitu na kutoa mchango mkubwa kwa huduma za afya, ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya matibabu wakati wa janga la COVID-19.

Kujitolea kwa wafanyakazi (Tuzo la Shaba)

Mpango wetu wa kujitolea kwa wafanyakazi, ambao huwawezesha wafanyakazi kushiriki katika miradi inayohusisha elimu, afya na mazingira, ulitambuliwa kwa kuendeleza utamaduni wa kutoa mchango kwa jamii.

Elimu/ufadhili wa masomo (Tuzo ya Dhahabu)

Mpango wa Exness wa ufadhili wa masomo ya teknolojia ya kifedha, ambao hutoa usaidizi wa kifedha kwa wanafunzi wenye vipaji katika nyanja za STEM, ulitambuliwa kwa kiwango cha juu kwa kusaidia kizazi kijacho cha wavumbuzi nchini Kupro.

"Tuzo hizi zinasherehekea juhudi nzuri za kila mtu aliyehusika—wajitoleaji wetu wenye shauku, wanafunzi wenye vipaji tunaofadhili na washirika wetu wenye maono katika Taasisi ya Teknolojia ya Kupro na Idara ya Misitu. Utambuzi sio heshima tu; ni motisha ya kuendelea kujenga mustakabali mwema kwa jamii zetu.”

Timu ya CSR ya Exness

Hitimisho

Kama mmoja wa brokers wakuu wa mali nyingi duniani, tumejitolea katika kutumia teknolojia si tu kwa ajili ya kutoa uzoefu wa biashara usio na hitilafu, bali pia kuchangia kwa njia yenye maana katika jamii tunakofanya kazi. Tuzo hizi zinathibitisha tena dhamira yetu ya kuleta mabadiliko chanya na tunapoingia kikamilifu mwaka wa 2025, timu yetu ya CSR tayari inatafuta njia mpya za kufanya dunia kuwa mahali bora.


Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.


Mwandishi:

Paul Reid

Paul Reid

Paul Reid ni mwandishi wa habari za kifedha aliyejitolea kufichua miunganisho ya kimsingi iliyofichwa ambayo inaweza kuwapa traders faida. Akilenga zaidi soko la hisa, hisia za Paul za kutambua mabadiliko makubwa ya kampuni zimethibitishwa vyema kutokana na kufuata masoko ya kifedha kwa zaidi ya muongo mmoja.