Jinsi ya kutumia indicator ya MACD kuboresha ujuzi wako wa biashara ya crypto

Antreas Themistokleous

Mtaalamu wa Kutrade wa Exness

Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.

Shiriki

Je, ungependa kuboresha ujuzi wako wa kutrade na kufaidika zaidi kutokana na Indicator ya MACD unapofanya trade ya crypto? Umepata nyenzo bora zaidi - soma mwongozo huu ili kupata maarifa ya kitaaluma.

Moving average convergence divergence (MACD) ni indicator ya uchanganuzi wa kiufundi inayotumika sana katika uchanganuzi wa kifedha. Iliyoundwa na Gerald Appel mwishoni mwa miaka ya 1970, MACD imekuwa mojawapo ya indicators maarufu zaidi ya kiufundi inayotumiwa na traders na wawekezaji. Uwezo wake wa kutambua mabadiliko ya trend yanayoweza kutokea na kutoa ishara ya ununuzi au uuzaji hufanya ipendwe na traders wa crypto. Lakini traders wengi bado wanajitahidi kuelewa kikamilifu uwezo kamili wa MACD na kuitumia kwa ufanisi.

Katika mwongozo huu, tutakuonyesha vipengele vya indicator ya MACD, kueleza ishara zake, kutoa vidokezo vinavyoweza kutumika, na kuchunguza uwezekano wa matumizi yake katika masharti tofauti ya soko.

Je, Indicator ya MACD ni nini?

Indicator ya MACD inajumuisha vipengele vitatu kuu: mstari wa MACD, mstari wa ishara, na histogramu. Ni muhimu kwamba kwanza uelewe jukumu la kila kipengele ili uweze kuelewa indicators za MACD kwa usahihi.

Mstari wa MACD

Mstari wa MACD hukokotolewa kwa kutoa exponential moving average (EMA) ya muda mrefu kutoka kwa EMA ya muda mfupi. Inaonyesha tofauti kati ya exponential moving averages hizo mbili na hutumiwa kutambua mabadiliko ya trend yanayoweza kutokea.

Mstari wa ishara

Mstari wa ishara ni moving average ya mstari wa MACD na kwa kawaida ni EMA ya siku 9. Huonyesha vyema mabadiliko ya mstari wa MACD na kutoa ishara za ununuzi au uuzaji wakati unaenda juu au chini ya mstari wa MACD.

Histogramu ya MACD

Histogramu ya MACD huonyesha tofauti kati ya mstari wa MACD na mstari wa ishara. Hutoa uwakilishi unaoonekana wa kukaribiana au kuachana kati ya mistari hiyo miwili, na kuonyesha nguvu ya trend.

Kukokotoa moving average convergence divergence

Ili kupata ufahamu kuhusu taratibu za msingi za MACD na kuelewa ishara zake vikamilifu wakati wa kutrade crypto, ni muhimu kuelewa jinsi MACD inavyokokotolewa. Ukokotoaji unajumuisha hatua zifuatazo:

Exponential moving average (EMA) ya muda mfupi

Unaweza kukokotoa EMA ya muda mfupi kwa kuzingatia zaidi data ya bei ya hivi majuzi, ambayo husababisha mabadiliko mengi kwenye mwenendo wa bei.

EMA ya muda mrefu

EMA ya muda mrefu hutoa uwakilishi unaoonekana vizuri wa mienendo ya bei kwa muda mrefu, na kupunguza kubadilika kwa mwenendo wa bei kwa muda mfupi.

Ukokotoaji wa mstari wa MACD

Unaweza kukokotoa mstari wa MACD kwa kutoa EMA ya muda mrefu kutoka kwa EMA ya muda mfupi.

Ukokotoaji wa mstari wa ishara

Mstari wa ishara kwa kawaida ni EMA ya siku 9 ya mstari wa MACD.

Ukokotoaji wa histogramu

Ili kuamua histogramu, sharti utoe mstari wa ishara kutoka kwa mstari wa MACD.

Jinsi ya kuelewa ishara za indicator ya MACD

Unaweza kuelewa ishara za ununuzi na uuzaji katika MACD kupitia mahali mistari ya ishara na MACD inavukana au kuachana.

Mahali mistari ya MACD na ishara inavukana

Kuvukana kwa mistari hutokea wakati mstari wa MACD unavukana na mstari wa ishara. Kuvukana kwa mistari kwa mwenendo wa kupanda hutokea wakati mstari wa MACD unavuka juu ya mstari wa ishara, na kuonyesha uwezekano wa kupanda kwa bei. Kwa upande mwingine, kuvukana kwa mistari kwa mwenendo wa kushuka hutokea wakati mstari wa MACD unavuka chini ya mstari wa ishara, na kuonyesha uwezekano wa kushuka kwa bei.

Kuachana

Kuachana kwa mistari kunarejelea tofauti kati ya mwenendo wa bei na indicator ya MACD. Kuachana chanya hutokea wakati hatua ya bei inafikia kiwango cha chini kilicho chini ya viwango vya chini zaidi vya awali huku mstari wa MACD ukifikia kiwango cha chini kilicho juu ya viwango vya chini zaidi vya awali, na hivyo kupendekeza uwezekano wa kubadilika kwa mwenendo wa trend. Kuachana hasi hutokea wakati hatua ya bei inafikia kiwango cha juu kilicho juu kuliko viwango vya juu zaidi vya awali huku mstari wa MACD ukifikia kiwango vya juu kilicho chini ya viwango vya juu zaidi vya awali, na kuonyesha uwezekano wa kubadilika kwa mwenendo wa trend.

Jinsi ya kutumia MACD kutambua trend

Mojawapo ya matumizi ya msingi ya indicator ya MACD ni kutambua trend. Kufahamu jinsi ya kuelewa ishara za ununuzi na uuzaji kwa MACD kwa usahihi kunaweza kusaidia kutambua points zinazowezekana za kuingia na kutoka kwenye soko.

Kuvukana kwa mistari kwa mienendo ya kupanda na kushika

Kuvukana kwa mstari wa MACD na mstari wa ishara kunaweza kutoa maarifa muhimu kuhusu mabadiliko ya trend na ishara zinazowezekana za ununuzi au uuzaji kwa fursa za biashara.

Kuvukana kwa mistari kwa mwenendo wa kupanda

Kuvukana kwa mistari ya ishara na MACD kwa mwenendo wa kupanda hutokea wakati mstari wa MACD unavuka juu ya mstari wa ishara. Ishara hii huonyesha kuwa trend ya muda mfupi inabadilika na kuanza kupanda, na kuonyesha uwezekano wa fursa ya kununua.

Kuvukana kwa mistari kwa mwenendo wa kushuka

Kuvukana kwa mistari ya ishara na MACD kwa mwenendo wa kushuka hutokea wakati mstari wa MACD unavuka chini ya mstari wa ishara. Ishara hii huonyesha kuwa trend ya muda mfupi inabadilika kuanza kushuka, na kuonyesha uwezekano wa fursa ya kuuza.

Ishara za uwongo na uthibitisho

Ni muhimu kuzingatia kutokea kwa ishara za uwongo na kutafuta uthibitisho kutoka kwa indicators zingine za uchanganuzi wa kiufundi au mitindo ya bei, kabla ya kuchukua hatua za biashara kulingana na kuvukana kwa mistari ya ishara ya MACD.

Kuachana chanya na hasi

Kuachana kati ya indicator ya MACD na bei kunaweza kukupa maarifa muhimu kuhusu mabadiliko ya trend yanayoweza kutokea.

Kuachana chanya

Kuachana chanya hutokea wakati bei inafikia kiwango cha chini kilicho chini ya viwango vya chini zaidi vya awali, huku mstari wa MACD ukifikia kiwango cha chini kilicho juu ya viwango vya chini zaidi vya awali. Ishara hii huonyesha kuwa shinikizo la mauzo linapungua, na kuna uwezekano wa mwelekeo wa trend kuanza kupanda.

Kuachana hasi

Kuachana hasi hutokea wakati bei inafikia kiwango cha juu kilicho juu ya viwango vya juu zaidi vya awali, huku mstari wa MACD ukifikia kiwango cha juu kilicho chini ya viwango vya juu zaidi vya awali. Ishara hii huonyesha kuwa mwenendo wa kupanda wa ununuzi unapungua, na kuna uwezekano wa trend kubadilika na kuanza kushuka.

Hii ni aina ya kuachana kwa mwenendo wa kushuka ambako kunaweza kuonyesha mwenendo wa kushuka unaotarajiwa.

Kutambua mabadiliko ya trend

Kuachana chanya na hasi kunaweza kutumika kama maonyo ya mapema kwa uwezekano wa mabadiliko ya trend. Hata hivyo, ni muhimu kuthibitisha ishara hizi kwa kutumia indicators zingine vya uchanganuzi wa kiufundi au mitindo ya bei kabla ya kufanya maamuzi ya biashara.

Kuamua nguvu ya trend

Unaweza kutumia histogramu ya MACD kutathmini nguvu ya trend.

Histogramu ya MACD

Histogramu ya MACD huonyesha tofauti kati ya mstari wa MACD na mstari wa ishara, na hutoa uwakilishi unaoonekana wa kukaribiana na kuachana kati ya mistari hiyo miwili. Histogramu ya MACD inayoongezeka inaonyesha mwenendo unaoongezeka, ilhali histogramu ya MACD inayopongua inaonyesha kupungua kwa mwenendo.

Mstari wa sufuri

Nafasi ya histogramu inayohusiana na mstari wa sufuri inaweza pia kutoa maarifa kuhusu nguvu ya trend. Thamani chanya juu ya mstari wa sufuri huonyesha trend ya kupanda, ilhali thamani hasi chini ya mstari wa sufuri huonyesha trend ya kushuka.

Je, uko tayari kujaribu indicator hii ya kiufundi kwenye Akaunti ya Demo au Standard Cent?

Kuboresha uchanganuzi wa MACD na indicators zingine katika crypto

Ingawa MACD ni indicator yenye nguvu ikiwa peke yake, unapoiunganisha na indicators zingine za kiufundi inaweza kukupa uchanganuzi wa kina zaidi wa soko la crypto.

Kuunganisha indicator ya MACD na moving averages

Kuunganisha moving average convergence divergence (MACD) na moving averages zingine kunaweza kutoa ishara za uthibitisho za ziada na kukusaidia kuchuja ishara za uwongo.

Golden cross na death cross

Golden cross hutokea wakati moving average ya muda mfupi ikivuka juu ya moving average ya muda mrefu (kwa mfano, MA ya siku 50) huvuka juu ya moving average ya muda mrefu (kwa mfano, MA ya siku 200), na kuashiria trend ya kupanda inayoweza kutokea. Death cross hutokea wakati moving average ya muda mfupi ikivuka chini ya moving average ya muda mrefu, kuonyesha trend ya kushuka inayoweza kutokea.

Chati ya muda mrefu yenye SMA ya siku 50 huonyesha moving average ya muda mfupi ikivuka juu ya moving average ya muda mrefu lakini yenye kuachana kwa mwenendo wa kushuka kutoka kwa MACD.

Moving averages kama support na resistance

Kutumia moving averages kama support au resistance levels kunaweza kutoa maarifa ya ziada kuhusu uwezekano wa mabadiliko ya bei inapounganishwa na ishara za MACD.

MACD na RSI

Kuunganisha MACD na relative strength index (RSI) kunaweza kuboresha usahihi wa uchanganuzi wa trend na kutambua hali zinazoweza kutokea za kununuliwa au kuuzwa kupita kiasi.

Hali ya kununuliwa na kuuzwa kupita kiasi

RSI inapofikia viwango vya kununuliwa kupita kiasi (kwa mfano, juu ya 70), na MACD ipate kuvukana kwa mistari kwa mwenendo wa kushuka au kuachana hasi, inapendekeza uwezekano wa kushuka kwa bei. Kwa upande mwingine, ikiwa RSI itaingia katika viwango vilivyouzwa kupita kiasi (kwa mfano, chini ya 30) na MACD huonyesha kuvukana kwa mistari kwa mwenendo wa kupanda au kuachana chanya, hii huonyesha uwezekano wa mwenendo wa kupanda.

Kukaribiana na kuachana

Unapoona kukaribiana kati ya indicator ya MACD na RSI, inaweza kukupa uthibitisho wa ziada wa trend ya sasa. Kwa upande mwingine, ukigundua kuachana, inaweza kuashiria mabadiliko yanayoweza kutokea katika trend.

MACD na kiwango

Kwa kuchanganua kiwango pamoja na MACD, unaweza kupata maarifa muhimu kuhusu nguvu ya mienendo ya bei na uwezekano wa mabadiliko ya trend.

Uthibitishaji wa kiwango

Wakati MACD inapata kuvukana kwa mistari kwa mwenendo wa kupanda au kuachana chanya ikifuatana na ongezeko kubwa la kiwango cha biashara, huwa inakupa uthibitisho wenye nguvu zaidi wa trend ya kupanda. Vile vile, kuvukana kwa mistari kwa mwenendo wa kushuka kwa MACD, au kuachana hasi na kuongezeka kwa kiwango, hukupa dalili kali ya trend ya kushuka inayoweza kutokea.

Kuachana kwa kiwango

Tofauti kati ya kiwango na indicator ya MACD inaweza kuashiria mabadiliko yanayoweza kutokea ya trend. Kwa mfano, ikiwa bei inafikia kiwango cha juu kilicho juu kuliko viwango vya juu zaidi vya awali huku kiwango kikipungua, inaweza kuonyesha kupungua kwa shinikizo la ununuzi na mabadiliko ya trend yanayoweza kutokea.

Vidokezo 5 vya kutumia indicator ya MACD katika trade ya crypto

Ili kufaidika zaidi kutokana na indicator ya MACD unapofanya trade ya cryptocurrencies, ni muhimu uitumie kwa njia ya vitendo na yenye nidhamu. Zingatia vidokezo vifuatavyo ili kuboresha maamuzi yako ya biashara ya crypto:

Kidokezo cha 1: Uchaguzi wa timeframe

Ishara za indicator ya MACD zinaweza kutofautiana kulingana na timeframe iliyotumika. Chagua timeframe inayolingana na mkakati na malengo yako ya biashara ya crypto. Timeframes fupi zaidi zinaweza kutoa ishara za mara kwa mara lakini zisizoaminiwa sana, ilhali timeframes refu hutoa ishara chache lakini zinazoweza kuaminiwa zaidi.

Kidokezo cha 2: Kuthibitisha ishara na indicators za ziada

Ili kuboresha usahihi wa indicator ya MACD, zingatia kutumia indicators zingine za kiufundi, kama vile mistari ya trend, support na resistance levels, au mitindo ya vinara, ili kuthibitisha ishara kabla ya kuanzisha trades zako za crypto. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupata orodha ya indicators na jinsi ya kuzitumia kwenye chati kupitia Eneo lako la Binafsi mara tu unapojisajili kwa akaunti ya kutrade ya Exness.

Kidokezo cha 3: Kuepuka masoko yenye misukosuko

Wakati wa volatility ya chini au masoko ambayo bei haisongi kwa viwango vikubwa, ishara za MACD zinaweza kosa kuaminika sana. Inashauriwa uwe mwangalifu na utafute uthibitishaji kutoka kwa indicators zingine au kungoja trends zilizo wazi zaidi kuibuka.

Kidokezo cha 4: Kuweka viwango vya stop loss na take profit

Utekelezaji wa hatua zinazofaa za udhibiti wa hatari ni muhimu wakati wa kutumia indicator ya MACD au indicator nyingine yeyote. Weka viwango vya stop loss na take profit kulingana na uvumilivu wako wa hatari na masharti ya soko yaliyopo ili kulinda mtaji wako na kufungia faida.

Kidokezo cha 5: Kujaribu na uboreshaji

Kabla ya kutekeleza sifa za indicator ya MACD katika trade ya moja kwa moja ya crypto, fanya majaribio kamili kwa hatua za kihistoria za bei na data ili kutathmini ufanisi wake katika masharti tofauti ya soko. Boresha vigezo vya indicator hii ya mwenendo kulingana na mtindo wako wa biashara na sifa za soko mahususi unalofanya trade. Katika Exness tunatoa aina mbalimbali za mali za kutrade. Kwa hivyo fanya utafiti wako na ulinganishe jinsi indicator hii inavyofanya kazi kwa kila mali.

Maswali yanayoulizwa sana

Indicator ya MACD peke yake ni zana muhimu kwa manufaa ya trader yeyote, lakini kama kwa indicators zote sio sahihi kabisa. Ili kupata mkakati bora zaidi kwanza unapaswa kuamua ungependa kuwa trader wa aina gani na ungependa kufungua trades mara ngapi. Ukigundua hilo basi unaweza kuanza kujaribu kuunganisha indicator ya MACD na zana zingine za kiufundi ili kukusaidia kufanya maamuzi sahihi ya kutrade. Muunganisho maarufu zaidi ni pamoja na moving averages (kufanya trade ya kuvukana kwa mstari wa ishara), RSI na indicators za kiwango.

Kwanza kabisa, indicators hizi zote mbili ni indicators za mwenendo zinazofuata trend, kumaanisha kwamba huwa zinachelewa kwa wakati, kwa hivyo hakuna indicator yoyote inayoweza kuaminiwa. Indicators hizi mbili ziko katika kategoria ya ‘indicator inayochelewa’, na hutumiwa na traders wageni na wenye uzoefu, hivyo kuaminiwa kwa indicator hakupaswi kupuuzwa. Sio muhimu kutofautisha ni 'indicator gani inayochelewa' ndiyo indicator bora au ya kiwango cha juu, lakini badala yake kuuliza ikiwa ni mkakati mzuri kuziunganisha. Kwa hili, jibu ni rahisi: ndio! Kuunganisha indicators hizi mbili ambazo haziwezi kuaminika na kuzirekebisha kwa mtindo wako wa biashara ndiyo njia bora zaidi.

Indicator ya moving average convergence divergence (MACD) ni indicator ya mwenendo inayotumika kufanya trade ya trends. Inajumuisha mistari miwili inayovukana ili kutoa ishara za biashara. Wakati MACD inavuka juu ya sufuri, inachukuliwa kuwa ya kupanda, na inapovuka chini ya sifuri, ya kushuka. Wakati wa kufanya trade ya safu, MACD inaweza kubadilika, na kwa ujumla inashauriwa kuepuka kutrade katika hali hii, kwa kuwa indicator hii hufanya kazi vizuri zaidi katika masoko ya kifedha yanayovuma. Kuachana kati ya MACD na mwenendo wa bei kunaweza kuwa ishara kali.

Histogramu ya MACD huonyesha pengo kati ya MACD na EMA yake ya siku 9, sio points za juu na za chini zaidi. Histogramu hukuwa katika eneo chanya wakati MACD iko juu kuliko EMA yake ya siku 9, na katika eneo hasi wakati iko chini. Mstari wa sufuri kwenye histogramu huonyesha wakati hakuna mwenendo.

Je, uko tayari kuboresha mkakati wako wa biashara wa MACD wa crypto?

Indicator ya MACD ni zana yenye nguvu ambayo inaweza kutoa maarifa muhimu katika trends za soko na fursa za biashara zinazoweza kutokea. Kwa kuelewa vipengele vyake, kueleza ishara zake, kuunganisha na indicators zingine za kiufundi, na kufuata vidokezo vya vitendo, unaweza kuboresha mchakato wako wa kufanya maamuzi na kuboresha matokeo yako ya biashara.

Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa hakuna indicator isiyo na upungufu. Ni jambo la busara kutekeleza udhibiti wa hatari wakati wote. Kwa mazoezi, uzoefu, na uboreshaji wa mara kwa mara, unaweza kutumia uwezo wa MACD kupata faida zaidi katika masoko ya kifedha.

Kwa hivyo, kumbatia indicator ya MACD, elewa upungufu wake, na ufungue uwezo wake wa kuboresha ujuzi wako wa biashara ya crypto. Kumbuka, kujifunza mara kwa mara na kuzoea ni muhimu katika ulimwengu unaobadilika wa biashara na uwekezaji.

Gundua uwezo wote wa indicator ya MACD pamoja na zana zingine za kiufundi, kwa kuzitumia kwenye akaunti yako ya Exness trade.

Shiriki


Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.