Indicator ya RSI kwa biashara ya stocks: mambo ya msingi na zaidi

Stanislav Bernukhov

Mtaalamu Mkuu wa Kutrade wa Exness

Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.

Shiriki

Katika makala haya, tutazungumza kuhusu utumiaji wa indicator ya RSI kwa biashara ya stocks. Relative strength index (RSI) ni kidhibiti kasi kinachotumiwa na traders na wawekezaji kutambua viwango vya kununuliwa na kuuzwa kupita kiasi katika stocks na instruments zingine za kifedha. Hukuwa kati ya 0 hadi 100 na hupima kasi na mabadiliko ya mienendo ya bei.

Vidhibiti kasi hufanya vyema katika masoko ambayo hutumia safu za biashara badala ya kuweka trends za muda mrefu. Ndiyo maana kutumia RSI kwa stocks kunaweza kuwa na changamoto, kwa kuwa mara nyingi stocks hudumisha trends kwa muda mrefu. Kwa hivyo, kutumia RSI bila makini, au bila indicators zingine za kiufundi za stocks kunaweza kusababisha hasara badala ya faida.

Makala haya hayatoi ushauri wowote wa uwekezaji au biashara. Badala yake, yanatoa nyenzo ya kielimu ili kukusaidia kuelewa zana ya RSI vyema.

Je, indicator ya RSI ni nini?

Relative strength index (RSI), ni kidhibiti kasi kinachotumika sana kwa uchanganuzi wa kiufundi wa biashara ya stock. Iliundwa na Welles Wilder mnamo Juni 1978, ambaye alielezea kwa kina njia yake ya ukokotoaji katika kitabu chake "New Concepts in Technical Trading Systems". Aina hii ya kidhibiti kasi ni zana ya uchanganuzi wa kiufundi ambayo hupima kasi na kiasi cha mabadiliko ya bei katika instrument ya kifedha. Inalinganisha wastani wa faida na hasara za amana katika kipindi fulani, na kukusaidia kubainisha nguvu na udhaifu wa mali.

Ukokotoaji wa RSI ni:

RSI = 100 − (100/(1=RS))

Unapata relative strength (RS) kwa kugawanya idadi ya wastani ya kufunga kwa kiwango cha juu kwa muda wa siku X kwa wastani wa idadi ya kufunga kwa kiwango cha chini katika kipindi sawa cha siku X. Welles Wilder alipendekeza matumizi ya RSI ya siku 14, ambayo inakubaliwa sana. Hata hivyo, bado una uwezo wa kuchagua idadi ya siku za kukokotoa.

Mambo ya msingi kuhusu indicator ya RSI

Indicator ya RSI huzunguka kati ya 0 na 100. Kwa ujumla, kiwango cha zaidi ya 70 cha RSI kinapendekeza kuwa stock imenunuliwa kupita kiasi. Hii inamaanisha kuwa kuna uwezekano wa bei kuanza kushuka. Kwa upande mwingine, kiwango cha chini ya 30 cha RSI kwenye chati ya bei kinaonyesha kuwa stock imeuzwa kupita kiasi. Hii inamaanisha kuwa kuna uwezekano wa bai kunze kupanda.

Indicator ya RSI imebadilika na kuanza kushuka kutoka sehemu ya kuuzwa kupita kiasi. Chanzo: Tradingview.com

Wakati ambapo RSI inavuka kiwango cha 70 au 20, unaweza kuiona kama ishara ya biashara. Hata hivyo, usitegemee tu ishara pekee katika kufanya trade yako.

Kutumia kuachana kati ya bei ya mali na indicator ya RSI kunaweza kukusaidia kupata picha wazi na ishara bora. Kuachana kati ya bei ya mali na indicator ya RSI ni ishara iliyothibitishwa, kumaanisha kuwa ina nguvu zaidi kuliko ishara ya kawaida ya RSI (inapovuka kiwango cha sehemu ya kuuzwa kupita kiasi, kwa mfano). Kuachana kati ya bei ya mali na indicator ya RSI, kwa hiyo, ni ya kuaminika zaidi na hutoa kiwango cha juu cha kupata faida; hata hivyo, huwa inaonekana kwa nadra sana.

Kuachana kati ya bei ya mali na relative strength index (RSI)

Unapotumia indicator ya relative strength index (RSI) kwa biashara ya stocks na ugundue kuachana kati ya RSI na mabadiliko ya bei ya stock, hii inaweza kumaanisha uwezekano mkubwa wa trades zako kufanikiwa wakati kuachana kwa kushuka kwa bei au kupanda kwa bei kunapotokea. Ikiwa stock unayotazama itafikia kiwango cha juu kilicho juu kuliko viwango vya juu zaidi vya awali lakini RSI ifikie kiwango cha juu kilicho chini kuliko viwango vya juu zaidi vya awali, inaweza kuonyesha trend ya kupanda inayodhoofika. Kwa upande mwingine, ikiwa stock inafikia kiwango cha chini kilicho chini ya viwango vya chini zaidi vya awali lakini RSI inafikia kiwango cha chini kilicho chini ya viwango vya chini zaidi vya awali, inaweza kupendekeza trend ya kushuka inayodhoofika.

Kuachana kati ya bei ya stock ya AAPL na indicator ya RSI. Chanzo: Tradingview.com

Kutumia indicators za kawaida za RSI kwa stocks

Hebu tuangalie majaribio ya mfumo wa biashara kulingana na indicator ya RSI katika matumizi kwa stock ya AAPL (Apple) iliyochukuliwa kutoka kwa jumuiya ya Trading View. Katika hali hii, mkakati unafaa kuweka position ikiwa imefunguliwa hadi utoe ishara katika mwelekeo tofauti.

Unapotumia RSI kwa njia rahisi zaidi (nunua wakati RSI inatoka sehemu ya kununuliwa kupita kiasi na kuuza inapotoka kwenye sehemu ya kuuzwa kupita kiasi) hutoa matokeo sawa katika timeframes zote - hasara ya mara kwa mara.

Majaribio ya mfumo wa biashara wa kiotomatiki kulingana na indicator ya RSI. Chanzo: Tradingview.com.

Hiyo hutokea kutokana na ukweli kwamba: stocks nyingi huonekana kubaki ndani ya awamu za kupanda kwa bei kwa muda mrefu, kinyume na jozi za sarafu, ambazo huonekana kubaki katika safu za biashara.

Vidhibiti kasi vyote vitaonyesha hali ya ‘kununuliwa kupita kiasi’ katika mwelekeo thabiti wa kupanda kwa bei, ambayo inapendekeza kufungua position ya uuzaji. - Kinyume chake, position ya ununuzi itafungwa mapema kwa kuwa soko huingia katika hali ya 'kununuliwa kupita kiasi', na trader anahitaji kufunga position hiyo.

Kutumia kuachana kati ya bei ya mali na RSI katika stocks

Unapata matokeo bora zaidi unapotumia kuachana kwa kupanda kwa bei au kwa kushuka kwa bei. Wakati thamani ya indicator ya RSI inabaki katika sehemu ya kununuliwa kupita kiasi kwa muda mrefu, pengine unapaswa kuepuka ishara za uuzaji, au utumie uthibitisho wa ziada, huku ukipendelea ishara za ununuzi.

Utawala wa ishara za ununuzi hukusaidia kudumisha positions katika mwelekeo wa trends. Katika mfano ulio hapa chini, utaona points za kuingia zikitolewa sio tu katika sehemu za kuuzwa kupita kiasi au sehemu za kununuliwa kupita kiasi. Huenda hilo likaonekana kukiuka kanuni za kitamaduni, lakini bei za kununuliwa/kuuzwa kupita kiasi hazipatikani kwa stocks nyingi. Kwa hivyo, idadi ya positions unazofanyia trade inaweza kuwa chini sana. Ndiyo maana wakati mwingine unaweza kukubali ishara hata nje ya sehemu hizi.

Majaribio ya mfumo wa biashara kulingana na kuachana kwa bei ya mali na RSI. Chanzo: Tradingview.com

Uthibitishaji wa ishara za RSI kwa stocks

Unaweza kutumia indicator ya RSI kama mwongozo wa trades zinazowezekana, kwani hivyo ndivyo inavyotumiwa mara nyingi, na sio kama kanuni kali ya kuingia. Ili kubainisha point ya kuingilia unapoanzisha trade, unaweza kutumia uthibitishaji.

Kwa mfano, mfumo wa kinara, kama vile ‘mfumo wa engulfing’, unaweza kuonyesha kuongezeka wa kasi.

Hivi ndivyo unavyoweza kutumia mfumo rahisi wa engulfing kwenye chati ya kinara ndani ya timeframe ya H1 ili kuthibitisha wakati wa kuingia kwenye trade.

Badala ya kufungua trade RSI inapotoa ishara, unaweza taka kusubiri mfumo unaotegemewa zaidi uonekane kisha ufanye uamuzi wako wa kuchukua hatua inayowezekana.

Muunganisho wa RSI na ishara za biashara mfumo wa engulfing wa kinara. Chanzo: Tradingview.com

Mipangilio bora zaidi ya RSI kwa mitindo ya biashara ya muda mfupi

Kulingana na takwimu, mitindo ya biashara ya muda mfupi kwa kawaida hufanya kazi vyema zaidi ikiwa na mipangilio ya RSI kati ya 20 na 50. Epuka kutumia vigezo vya chini ya 10 kwa kuwa indicators zako za RSI zinaweza kuwa nyeti sana, kuashiria kimakosa hali ya soko ya kununuliwa au kuuzwa kupita kiasi. Hata hivyo, jaribu mipangilio hii kila mara kwa instrument yako mahususi ya biashara ili kuhakikisha kuwa ina ufanisi.

Mipangilio bora zaidi ya RSI kwa mitindo ya biashara ya muda mrefu

Kama trader wa muda mrefu, kutumia kigezo cha 50 kwa RSI kunaweza kukusaidia kuzuia kufanya biashara kupita kiasi. Pia ni muhimu kutumia kigezo hiki kwa timeframes ndefu kama vile chati za kila siku. Kumbuka kufafanua vigezo sahihi kupitia majaribio. Traders wa kitaaluma mara chache hubadilisha vigezo vya indicators zao ili kuepuka utumiaji kupita kiasi.

Faida na hasara za kutumia indicator ya RSI kwa biashara ya stock

Katika sehemu hii, tunaangazia uwezo na udhaifu wa kutumia relative strength index (RSI) kwa biashara ya stock. Kwa upande wa faida, zana hii ya uchanganuzi wa kiufundi inaweza kusaidia kutambua points nzuri za kuingia na kutoa kiwango cha juu cha kupata faida na pia ni rahisi kuitumia. Hata hivyo, si kamili: mara nyingi inaweza kutoa ishara za uwongo, huenda isiongeze maarifa zaidi ya bei na kiwango, na ufanisi wake unaweza kutofautiana katika timeframes tofauti.

Faida za indicator ya RSI katika biashara ya stock

  1. Mara nyingi stocks huanzisha trends za muda mrefu za kupanda kwa bei. Indicator ya RSI inaweza kusaidia kupata point nzuri ya kujiunga na trends kama hizi.
  2. Ni rahisi kutumia indicator ya RSI. Mikakati ya kimsingi ya biashara ya RSI haihitaji uwe na kiwango cha juu cha ujuzi wa biashara.
  3. Ishara za RSI hazihitaji kuitikia kwa haraka kutoka kwako, kama trader, na kwa kawaida hukupa muda wa kutosha kutayarisha na kutekeleza trade.
  4. RSI inalenga ishara za biashara za bei kurejea kwenye wastani wa kihistoria, ambazo hutokea mara nyingi zaidi kuliko ishara za trend. Kwa maneno mengine, ikiwa itatumika kwa usahihi, RSI inaweza kukusaidia kufikia kiwango cha juu cha faida.
  5. Mikakati mingi ya RSI tayari imejaribiwa na matokeo yanapatikana hadharani. Hizi ni pamoja na matumizi yao kwa stocks. Kwa hivyo, hauhitaji ‘kujaribu tena’ au kupitia mchakato mgumu wa kujaribu na kukosa wakati wa kutumia indicator ya RSI.

Hasara za indicator ya RSI katika biashara ya stock

  1. RSI haifanyi kazi vizuri katika trends za muda mrefu, na soko la stock linajulikana kwa trends za kupanda kwa bei kwa muda mrefu. Kwa mfano, RSI inaweza kutoa ishara nyingi za uwongo za kupinga trend, ikiwa itatumika kwa stockambayo bei yake inapanda mara kwa mara.
  2. RSI ni indicator tu, kumaanisha kuwa inatokana na bei. Ikiwa wewe ni trader anayeanza, inaweza kukusaidia kupanga data, lakini haiwezi kuongeza chochote kipya ili kukuongoza katika kufanya maamuzi zaidi ya bei pamoja na kiwango.
  3. RSI hufanya kazi kwa kutumia bei kurejea kwenye wastani wa kihistoria, ambayo inamaanisha kuwa inaweza kusaidia trades kufikia kiwango cha juu au cha chini cha hatua ya bei. Mikakati ya bei kurejea kwenye wastani wa kihistoria si kamilifu na inaweza kuleta hasara ikiwa bei ya stock itabadilika haraka au itaendelea kuelekea upande mmoja, hasa kwa gaps.
  4. RSI haiathiriwi sana kwa hatua ya bei. Inaweza kukupa ishara mapema sana.
  5. Mikakati ya RSI inaweza kufanya kazi kwa njia tofauti katika timeframes tofauti, kwa hivyo sharti utumie utafiti wa kina kabla ya kuzitumia.

Maswali yanayoulizwa sana

Mkakati bora zaidi unaofaa kwa kutumia zana hii ya uchanganuzi wa kiufundi kwa stocks labda ni kuachana kwa bei ya mali na RSI. Mkakati huu wa biashara wa RSI unaweza kuboresha usahihi na muda wako, hivyo kukuruhusu kuona mabadiliko katika hatua ya bei mapema kabisa.

Kwa kuwa RSI kwa kawaida huangazia trades za bei kurejea kwenye wastani wa kihistoria, ni jambo la busara kuchuja trends thabiti za bei, ili kuepuka kuwa katika upande usiofaa wa soko. Kwa hivyo, RSI huingiana vizuri kama indicator kuu pamoja na moving averages au moving average convergence divergence, ambayo inaweza kukusaidia katika kutambua trends.

Usahihi wa indicator hii hutegemea mambo mbalimbali. Kwa kawaida, ungeweza kutumia relative strength index kwa biashara za bei kurejea kwenye wastani wa kihistoria, ambazo kwa kawaida hutokea katika zaidi ya 60% ya matokeo. Hata hivyo, sharti ukumbuke kwamba indicators za kiufundi ni zana tu. Utendaji wako wa mwisho unategemea mambo kama vile kuweka kiwango kizuri cha kusitisha, hatari, usimamizi wa pesa na kuweka malengo.

Kwa ujumla, RSI imeundwa kwa ajili ya kufanya kazi kwa timeframes ndogo hadi za kati, kama vile chati za kila saa, chati za dakika 30 na chati za saa nne. Ingawa hakuna vikwazo kwa utumiaji wa indicator hii, trader anapaswa kukumbuka kuwa kadiri timeframe ilivyo kubwa, ndivyo soko linaweza kuwa na ‘trends’ zaidi. Indicator ya RSI hufanya kazi vizuri zaidi - katika kutambua masharti ya kununuliwa au kuuzwa kupita kiasi kwa muda mfupi, ambayo inamaanisha kufanya kazi katika safu ya biashara.

Timeframes za juu, kama vile D1, hutoa mzunguko mdogo na mwenendo wa juu. Ndio maana kutumia indicator ya mwenendo itakuwa vyema kwa timeframes kubwa.

Kwa upande mwingine, mikakati ya biashara ya RSI iliyoundwa kwa timeframes ndogo, kama vile chati za dakika 1 au 5, pia ni ya kutiliwa shaka, kwani uwezekano wa faida kwa ishara zozote za RSI utakuwa chini sana: traders wanaweza kuwa na gharama nyingi za biashara na faida ndogo. Kwa hivyo, timeframe bora kwa RSI labda ni kati ya M15 na H4.

‘mkakati wa RSI wa vipindi viwili’ uliundwa kwa ajili ya biashara ya stock na Larry Connors. Ni tofauti ya bei kurejea kwenye wastani wa kihistoria na kigezo cha pili cha RSI. Eneo la chini ya 10 linachukuliwa kuwa sehemu ya kuuzwa kupita kiasi, na kwa kawaida, traders wanaweza kutafuta fursa za kununua chini ya masharti hayo. Kinyume chake, ikiwa bei itapanda zaidi ya 90, traders wanaweza kutafuta ishara za kuuza.

Kama mkakati mwingine wowote wa bei kurejea kwenye wastani wa kihistoria, huu haukuundwa ili kubainisha kiwango cha juu na chini, bali kujiunga na trend inayotawala kutoka kwa kubadilika kwa bei. Kwa trends zifuatazo, ni bora kutumia indicators za mwenendo, kama vile moving averages.

Je, ungependa kufanya biashara ya stock kwa kutumia indicator ya RSI?

Kumbuka, hakuna indicator, ikiwa ni pamoja na relative strength index (RSI), inayopaswa kuwa nyenzo yako ya kipekee ya kufanya maamuzi ya biashara.

Pia unahitaji kuzingatia vipengele kama vile masharti ya soko na jinsi bei ya mali ilivyo karibu na support au resistance levels.

Kwa stocks, ni muhimu kutodumisha position katika kipindi cha kufungwa cha uchapishaji wa ripoti ya mapato. Bei za stock zinaweza kubadilika kwa kiasi kikubwa katika tukio la mapato yasiyotarajiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufanya biashara ya CFD kwa stocks hapa.

Chukulia indicator hii kama mwongozo, na si kama kibashiri ‘kinachokuhakikishia’ mapato. Utendaji wa awali wa indicator yoyote hauhakikishi mafanikio ya baadaye.

Je, uko tayari kuanza kufanya biashara ya stock na kujaribu RSI? Fungua akaunti katika Exness leo.

Shiriki


Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.